SIKU YA KISWAHILI DUNIANI

Kiswahili kwa Amani, Ustawi na Utangamano wa Kikanda

KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI TAREHE 6 JULAI, 2022 ZANZIBAR, TANZANIA

Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki itaadhimisha siku hii kwa namna ya pakee. Kwanza ni kwa machapisho ya Kiswahili, pili ni Kongamano la Kiswahili litakalowakutanisha wataalamu na wadau wa lugha ya Kiswahili, na baada ya yote ni usiku wa Mswahili...hapa tutaona mavazi ya Mswahili na mambo mengine mengi ya kiutamaduni.